Monday, September 5, 2016

INTRODUCTION TO COMPUTER

IFAHAMU KOMPYUTA


UNAFAHAMU NINI KUHUSU KOMPYUTA?
Na Mohamed Ponera <link >Kupitia wikipidia

Kompyuta ni mashine inayotumia data kwa njia tofauti kutokana na maagizo zilizoandikwa kwenye bidhaa pepe ( software). hivyo basi Kompyuta  ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa (Data), kufanyia kazi na kutoa matokea ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information).
Teknolojia hii ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.
Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu


Aina za kompyuta

Kuna aina kuu tatu za kompyuta, nazo ni kama ifuatavyo:-
1. Digital Computers: Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kufanyia hesabu pamoja na kazi za kutumia akili.Kompyuta za aina hii ndio ambazo zipo katika matumizi hasa katika Dunia hii ya mabadiliko ya teknolojia.
2. Analog Computers:
Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kupokea taarifa (Data) kama zile za kusomea hali ya hewa, kupimia mishipa ya damu na kupimia kiwango cha chumvi kwenye maji.
3. Hybrid Computers:
Kompyuta hizi zinafanana na zile zilizotangulia kutajwa hapo mwanzo, nazo zinatumika kwa ajili ya kutafutia taarifa (Data) kutoka kwa binadamu moja kwa moja na kupitia mandishi na vipimo.


Aina za digital kompyuta

Super Computers:
Takriban zinapatikana sehemu zote duniani, na zinauwezo na nafasi kubwa ya kuhifadhi vitu vingi (Information) na zinatumika kwa ajili ya kazi za kijeshi na sehemu za ukaguzi, pia kompyuta hizi haziruhusiwi kuhamishwa nje ya nchi na kujua jinsi gani zinatumika. Na zinasifika kuwa na umbile la kati na kati, pia zina uwezo mkubwa na uwepesi wa hali ya juu.

Mainframe Computers:
Nazo ni kompyuta zenye umbile kubwa, na zilianza kudhihiri kwake katika mwanzo wa miaka ya hamsini, nazinasifika kwa uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu na pia uwepesi wa hali ya juu.
 
Mini Computers:
Aina hizi za kompyuta zilidhihiri katika kipindi cha miaka ya sitini.Ni kompyuta zenye umbile dogo kuliko zile zilizotangulia kutajwa,na ni bora kwa kuunganishia kompyuta nyengine zinazotumika viwandani na ndani ya nchi.
Micro Computers:
Aina hii ya kompyuta inakusanya aina zifuatazo:-
Personal Computers (PCs) ambazo ni maalumu kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja tu. Home Computers, Portable Computers: Nazo ni kompyuta za kubeba mkononi, ambazo zimegawanyika katika aina zifuatazo:-
1. Laptop.







2. Notebook.
3. Palmtop.






Kazi za msingi za kompyuta
  1. Kazi za uingizaji (Input).
  2. Kazi za uwendeshaji au ufanyishaji (Proccessing).
  3. Kazi za utoaji (Output).
  4. Kazi za kuhifadhi (Storege)

Matumizi ya kompyuta

Elimu:
Kutokana na kuendelea kwa elimu ya teknolojia imetusaidia sana kujifunza mambo mbali mbali kupitia kompyuta, ambapo unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa haraka tena kwa njia tofauti, pia unaweza kutumia kompyuta kwa ajili ya kufanya majadiliano ya kielimu, pia unaweza kuandaa vipindi mbali mbali vya masomo na kufundishia elimu tofauti. Pia unaweza kuonyeshea filamu zenye mafundisho mazuri, kama kuonyesha filamu zenye elimu ya jeografia na sayansi ya mifugo na kilimo, kuonyesha sehemu muhimu za nchi yetu, kuonyesha athari za nchi ambazo ndiyo sehemu kuu zinazotuletea fedha za kigeni katika nchi yetu, na kuonyesha picha za maendeleo katika sekta mbali mbali za nchi yetu, pia kuonyeshea mila na tamaduni za taifa letu la Tanzania na mataifa mengine mbali mbali duniani n.k.
Michezo:
Kompyuta zimeandaliwa ndani yake programu mbali mbali zenye michezo tofauti, ambayo inaweza kutumika na watu mbali mbali kutofautiana na umri wao, na ambayo inajulikana kama moja ya kazi za kukuza kipaji na kuchangamsha akili, na ni sehemu moja wapo ya kuburudisha nafsi.
Ufundi:
Kompyuta zinaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia kazi za ufundi, kama kuchora ramani ya nyumba na mazingira ya nje ya nyumba, kutengenezea picha kwa kuibadilisha na kuiremba na kuifanya ionekane katika sura nyengine ambayo tofauti na ile ya asili.
Mawasiliano:
Kompyuta inaweza kutumika kwa ajili ya kufanyia mawasiliano kupitia mtandao wa (Internet) ambao leo hii ndiyo umeshika nafasi kubwa sana ya mawasiliano kuliko kitu chengine ulimwenguni, kama kuwasiliana kwa kutumiana ujumbe wa barua pepe (E-mail) ambayo ni rahisi na inafika haraka kuliko barua za kupitia posta, pia kwa kutumia barua pepe hakuna haja ya kufikiria sehemu aliko mtu America au Asia au sehemu nyengine duniani, kuwasiliana kwa maneno ya maandishi (Chat), pia kuwasiliana kwa maneno ya sauti na kuonekana picha.
Usafirishaji:
Kwa kutumia kompyuta unaweza kuendeshea kazi za usafirishaji katika vituo vikuu vya usafirishaji, kama usafiri wa ardhini (mabasi, metro na treni), usafiri wa majini (meli), na usafiri wa angani (ndege).
Matumizi ya kiwandani:
Kama kuendeshea mashine viwandani kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbali mbali, kama kutengenezea magari, kuzalishia umeme na kutengenezea bidhaa nyengine za kawaida kama nguo mazulia n.k.
Matumizi ya benki:
Kama ilivyokuwa ada na kawaida hivi sasa kutumia kompyuta kwa ajili ya kuendeshea kazi za benki,kwa ajili kurahisisha kazi za mahesabu.
Kufanyia matibabu:
Kompyuta zimekuwa na matumizi makubwa na muhimu sana katika kufanyia uchunguzi na matibabu hospitalini, kama kuchunguza na kuelekeza dawa ya kutibu ugonjwa uliyoonekana, pia kupimia na kujaribia mimba na kutoa maelekezo kuhusiana na siku na tarehe ya kujifungua.

Kazi za kompyuta

1. Kuhifadhi vitu (Data):
Kama ilivyotanguliwa kusemwa hapo awali kuwa kompyuta ni chombo pekee chenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu, na mpaka hivi sasa bado hakijapatikana chombo chengine chenye uwezo mkubwa wa kuhifadhia vitu zaidi ya kompyuta.
2. kuonyeshea matokeo ya vitu (Data na Information):
Kutokana na kuendelea elimu ya teknolojia imeweza kuturahisishia kazi zetu nyingi ambazo tulikuwa tunazifanya kupitia vyombo mbali mbali, na kila chombo kilikuwa na kazi yake maalumu, tofauti na kompyuta ambapo mtu anaweza kuanzisha au kutengeneza kitu na wakati huo huo anaweza kukionyesha kwa kutumia kompyuta yenyewe, yaani kuonyesha ufanisi na sura nzuri ya kitu kilichofanyika.

Sehemu kuu mbili za kompyuta

1. Sehemu zinazoshikika (Hardware) Sehemu zinazoshikika (Hardware), ni aina zote za vifaa vya kompyuta, navyo vimegawanyika katika sehemu kuu tatu.
Vifaa vya kuingizia vitu (Input devices):
  1. kibodi (keyboard)
  2. Mausi (Mouse)
  3. Skana (Scanner)
  4. Makrofoni (Microphone)
  5. Kamera (Camera)
1. KIBODI (KEYBOARD):
Kibodi inatumika kwa ajili ya kuingizia herufi, namba, alama na michoro, nayo imegawanyika katika sehemu kuu nne, nazo ni kama ifuatavyo: Funguo za kuandikia (Typewriter keys), funguo za kuhama (Movement keys), funguo za namba pamoja na michoro mingine (Numeric keys) na funguo za kazi Function keys).
elewa maana ya vitufe vya kibodi ya kompyuta
Home natumika kwa ajili ya kuhamia mwanzo wa mstari
End Inatumika kwa ajili ya kuhamia mwisho wa mstari.
Pg Up Inatumika kwa ajili ya kuhamia juu ya mstari. 
Pg Dn Inatumika kwa ajili ya kuhamia chini ya mstari.                                                                           Num lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia namba na michoro.                                         Caps lock Inatumika kwa ajili ya kufunga na kufungulia.                                                                    Enter Inatumika kwa ajili ya kutekeleza amri, au kuanzisha fungu la maneno kwenye ukurasa..         Del “Delete” Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya mbele yake.                                                    “Back space" Inatumika kwa ajili ya kufuta herufi ya nyuma yake.                                                  Space “Space bar” Inatumika kwa ajili ya kuweka masafa kati ya maneno.                                         Esc “Escape” Inatumika kwa ajili ya kuacha kutekeleza amri.                                                                 Tab Inatumika kwa ajili ya kuwacha masafa maalumu tofauti na ya kawaida (Normal).
Ctrl “Control” inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.                                                                                                                                                               Alt inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.              Shift inatumika daima pamoja na ufunguo mwengine kwa ajili ya kutekeleza amri maalumu.  Alt-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia lugha.                                                                              Ctrl-Shift Inatumika kwa ajili ya kubadilishia mwelekeo ndani ya ukurasa (kulia au kushoto)     Print screen Inatumika kwa ajili ya kupiga picha kitu chochote kwenye kompyuta.
Ctrl-Alt-Del Inatumika kwa ajili ya kuwasha upya kompyuta.
3. MAUSI (MOUSE):
Kuna vitufe viwili kwenye kila mausi, kitufe cha upande wa kushoto (Left click) kinatumika kufungulia windozi, programu na kuchagulia maandishi, maneno na picha, na kitufe cha upande wa kulia (Right click) kinatumika kufungulia orodha ya mapendekezo ya kazi.
 
4. SKANA (SCANNER)
Skana inatumika kwa ajili ya kuingizia picha ndani ya kompyuta. Na kitu chochote kile kinachoingia ndani ya kompyuta kwa njia ya skana kinapewa sifa ya picha.
 
5. MAKROFONI (MICROPHONE):
Makrofoni inatumika kwa ajili ya kuingizia sauti ndani ya kompyuta.
 
6. KAMERA (CAMERA):
Kamera inatumika kwa ajili ya kupigia picha na kuingiza ndani ya kompyuta.
 

Viafaa vya kutolea vitu (Output devices):
1. SKRINI (SCREEN):
Skrini inatumika kwa ajili ya kuonyeshea matokeo ya vitu vilivyofanyika ndani ya kompyuta.
 
2. KITOA SAUTI (SPEAKER):
Kipaza sauti kinatumika kwa ajili ya kutolea sauti kutoka ndani ya kompyuta.

3. PRINTA (PRNTER):
Printa inatumika kwa ajili ya kutolea vitu vya maandishi au picha kwenye kompyuta kwa njia ya karatasi (kuchapisha).

4. PLOTA (PLOTER):
Plota ni ni chombo kinachotumika kwa ajili ya kutolea vitu, ambacho kinafanana na printa katika ufanisi wake wa kazi, lakini umbile lake ni kubwa kuliko printa, na kinatumika kwa ajili ya kuchapishia picha na michoro ya kiufundi, pia kinaweza kutumika kwa ajili ya kuchapisha maandishi kama herufi namba na alama.

2. Sehemu zisizoshikika (Software):
Kompyuta haiwezi kufanya kazi mpaka kipatikane kitu kinachoitwa software, ambocho kinawakilisha programu zinazoendesha kompyuta. Na programu hizo zimegawanyika katika sehemu kuu mbili:-
1. Programu za kuendeshea kompyuta (operating systems), programu hizo zinaitwa windows, na kuna aina nyingi za windows kulingana na toleo lake na ubora wake, kwani kila siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo tunapozidi kupokea programu nyingine za windows na zenye ubora zaidi kuliko zile zamani.

Kompyuta ya kisasa
  1. Kiwamba (skrini)
  2. Bao kuu(motherboard)
  3. CPU (bongo kuu)
  4. RAM (Kumbukumbu ya muda)
  5. Kadi za nyongeza kama vile kadi mchoro n.k.
  6. Ugawi wa umeme(power supply)
  7. Kiendeshi CD(CD/DVD drive)
  8. Kiendeshi diski kuu (HDD drive)
  9. Baobonye(keyboard)
  10. Puku(mouse)
vifaa vya kuendeshea vifaa vya kuingizia na kutolea vitu:
Vifaa hivi vipo ndani ya chombo kiitwacho (CPU) kifupi cha Central Processing Unit, ambacho ni kiini cha kompyuta na ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vyote vya kompyuta na kutoa maelekezo yote. Na CPU. ni sehemu kuu ya nguvu ya kompyuta, au kitovu cha kompyuta.Embu kwa kifupi tuangalie kazi kuu za CPU
Kazi za CPU:
1. Kutawala (Control): Ndani ya madhabodi (Motherboard) kinapatikana kifaa kinachoitwa (Bios) kifupi cha Basic Input Output System, ambacho ndicho kinachofanya kazi ya kuviendesha vifaa vya kuingizia na kutolea vitu. Na ni vigumu kufuta au kurekebisha vitu vilivyomo ndani ya kifaa hicho kwani vinazingatiwa ni vitu vya kusomea tu na si kwa kazi nyingine.
2. akili na mahesabu (arithmetic logical):
Kazi za mahesabu ni kazi zote zinazofanyika na hesabu, kama vile kutoa, Kujumlisha, kuzidisha na kugawanya. Na za akili

WINDOWS XP:

Windows Xp inazingatiwa kuwa ni miongoni mwa Windows za kisasa zenye kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko zile za zamani, kama Windows 95, Windows 98 na Windows Millenium.

  1. Uwepesi wa kuanza na kumaliza kutumia.
  2. Uwezo wa kutumia lugha mbili mfano kingereza na kiarabu, pia uwezo wa kubadilisha lugha hizo na kuweka nyengine.
  3. Kufungua kurasa kwa haraka.
  4. Uwezo wa kuendesha programu zaidi ya moja katika wakati mmoja.(Multitasking)
  5. Uwezo wa kuhifadhi vitufe (files) vilivyofutwa katika recycle bin.
  6. Uwezo wa kufanya kazi katika mdahalishi (Network) kwa haraka.
  7. Uwezo wa kubadilishana vitu (Data) kati ya programu tofauti.
  8. Kutumia majina marefu zaidi ya herufi 255 katika jina la faili moja.
  9. Haraka na uwepesi katika utekelezaji.
  10. Vifaa vya kisasa vinavyowezesha kufanya kazi katika net.
  11. Uwezo wa kutambua idadi nyingi ya vyombo vilivyounganishwa ndani ya kumpyuta.
  12. kuwepo kwa picha nyingi zenye kuvutia kwa ajili ya kupamba skirini (Backgrounds).
KUANZA KUTUMIA WINDOWS:
Kabla ya kuanza kutumia windows unatakiwa kufanya mambo yafuatayo:-
1. Kuhakikisha waya wa umeme umeshaunganisha kwenye kompyuta yako.
2. Kufungua kompyuta kwa kutumia sehemu inayoitwa power.
3. Kusubiri mpaka idhihiri sehemu inayoitwa desktop.


NI VIPI WATU WANAIBIWA TAARIFA ZAO KWA SABABU YA KUUZA KOMPYUTA ZAO BILA KUSAFISHA
 Kuna watu wamekuwa wakipata hasara katika makampuni yao au hata watu binafsi kutokana na kuuza kompyuta zao kwa watu wengine .Uuzaji wa kompyuta bila kuisafisha umeawafanya watu wengi kuibiwa kumbukumbu zao za siri bila wao kufahamu na kumbukumbu hizo zinapoangukia kwenye mikono ya watu wabaya inakuwa hasara kwa aliyeuza kompyuta hiyo.JeUnataka kuuza kompyuta yako na kununua mpya,lakini kwenye kompyuta yako kuna kumbukumbu nyingi za muhimu ambazo usingependa mtu mwingine yeyote azipate wala kuziona.Je utafanya nini?

Wapo ambao wamekuwa wakitumia mbinu za kawaida kufuta data kwenye kompyuta zao kama Kufuta(delete) au kuformat .Utafuta kila kitu kwa kubonyeza "Delete" halafu kwenda jalala(Recycle bin) kufuta kila kitu Au utaamua kuformat na kuifanya kompyuta yako kufuta kila kitu.Hii Haitasaidia Swali ni je njia ipi ni sahihi ya kusafisha kompyuta yako kabla ya kuiuza?

 Majibu ni mengi na inategemea na ufahamu wa muhusika,ila ukweli ni kuwa kwa njia zote mbili za hapo juu hakuna hata njia moja iliyo salama,kwani kama utatumia njia kama hizo na ukamuuzia
mtu mwenye utaalam wa kompyuta,basi ataweza kuzirudisha(recover) kumbukumbu zote ambazo mwenyewe ilizani zimefutika.Kbla ya kujua njia za kujikinga basi tuone ni kwa namna gani kompyuta inatunza kumbukumbu.

 Jinsi kompyuta  inavyohifadhi kumbukumbu

Wengi wetu wanaweza wakawa wameshaanza kujiuliza,inakuwaje sio salama wakati nimeshafuta kila kitu toka kwenye kompyuta? Je mtu ataweza vipi kuona mafaili ambayo tayari nimeshayafuta?
Ukweli ni kuwa,kwa mujibu wa uhifadhi wa kumbukumbu kwenye kompyuta.Pindi unapofuta au kufanya format(kuweka mtambo endeshi(OS) mpya),sio kweli unayafuta moja kwa moja mafaili na kumbukumbu
toka kwenye kompyuta yako.Kitu kinachofanyika ni kuwa unaondoa taswira yake kwenye uso wa mbele wa hard disk hivyo kukufanya wewe uone kama umeyafuta ila bado yanaendelea kuwepo kwenye disk yako.Na hii ndio maana kama kunatokea kesi,wataalam wa uchunguzi wa makosa ya kompyuta(Computer Forensic) huchukua kompyuta yako kwa ajili ya kuifanyia uchunguzi.


 Siku hizi kuna program nyingi sana ambazo zina uwezo wa kurudisha mafaili hata yale yaliyokuwepo kipindi ulipoinunua kompyuta kwa siku ya kwanza, mara nyingi jinsi gani unaweza kuyarudisha
hayo mafaili hutegemea elimu ya mtu anayefanya hizo kazi ya kuyarudisha,kwani kazi ya kuyarudisha haya mafaili huwa ngumu kutegemeana na jinsi mafaili hayo yalivyofutwa.Mfano faili
lililofutwa kwa kubonyeza "Delete" ni rahisi zaidi kulirudisha kuliko lile lililofutwa kwa kuformat kopyuta, vilevile huwa ngumu zaidi kama mtumiajai alifanya mgawanyo wa hard disk (partition) baada ya kuformat.
 Hivyo leo hii nitakuonehsha njia thabiti za kufuta kumbukumbu toka kwenye kompyuta unayotaka kuiuza ili kuhakikisha unakuwa salama zaidi.

Nitafutaje kumbukumbu moja kwa moja toka kwenye kompyuta?

Takwimu zinaonesha kuwa mtu mmoja kati ya wanne wamekuwa wakiibiwa siri zao kutokana na kuuza kompyuta bila kufuta kumbukumbu,hivyo kama wewe hutaki kuingia kwenye hilo kundi basi unaweza kufuata hatua zifuatazo.
1.Chukua ile CD uliyopewa pindi uliponunua kompyuta yako,ambapo nyingi huitwa recovery CD.Kama umepoteza hii CD au haukupewa pindi uliponunua kompyuta,basi nenda online na tafuta programu zinazotumika kufuta kumbukumbu(disk-wiping program). Programu hizi zipo nyingi ila binafsi nimewahi kutumia Darik's Boot and Nuke (DBAN) hivyo nakushauri uijaribu hii.

2.Tumia programu kama Nero au yoyote uliyoizoea kuchoma hayo mafaili ya hii programu kwenye CD,kumbuka kuchagua mtindo wa Bootable CD.

3.Weka CD kwenye kompyuta yako halafu irestart. Kompyuta inatakiwa kuitambua hiyo CD pindi tu inapowaka,kutatokea ujumbe kwenye kioo unaosomeka "press any key to boot from CD." Hapo bonyeza kitu chochote kwenye keyboard yako.

Kumbuka: Kama hautouona huu ujumbe unaosomeka"boot from CD" inawezekanika kabisa umekosea katika kuchoma hiyo CD yako,unatakiwa kuichoka kama "Bootable CD".

Jaribu tena au wasiliana na mtaalamu wa IT aliye karibu nawe. Kama una uhakika kabisa uliichoma kama Bootable CD,basi inawezekana kuna mabadiliko unatakiwa kuyafanya  ili kuiwezesha kompyuta kuitambua CD,haya kwa wasio na utaalam inabidi wawatafute wenye utaalam kidogo ili wakusaidie kubadilisha utaratibu wa BIOS.

Kama unataka kujaribu mwenyewe,basi kompyuta inapowaka tu bonyeza "Delete",baada ya hapo fuata maelekezo na kuingia kwenye "Boot Sequence",iweke CD or DVD kuwa ya juu kabisa kabla ya Hard drive,hapo mambo yatakuwa sawia.


4.Fuata maelekezo utakayopewa na hiyo programu,mara nyingi huchukua masaa kadhaa hadi siku mpaka kufuta kila kitu kilichopo kwenye kompyuta yako.
 Kama haujiamini,njia salama kwa 100% ni kutoa hard disk na kuiweka kwenye jiwe,halafu chukua nyundo na ivunjevunje au imwagie petrol na kuichoma moto.


Baada ya hapo basi kompyuta yako itakuwa mbichi kabisa na unaweza kuiuza bila utata wala hofu juu ya kumbukumbuku wala usalama wako.

3 comments: